Mpanda FM

Wazazi Chanzo cha Watoto Kujihusisha na Biashara Muda wa Masomo

4 October 2022, 5:49 am

KATAVI

Wazazi kutohusika kwenye malezi ya watoto wao imekuwa ni chanzo cha watoto kujihusisha kwenye shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato, muda ambao watoto hao walipaswa kuwa shule.

Wakizungumza na mpanda Radio fm baadhi ya watoto wakiwa kwenye shughuli za kujitafutia kipato  wamesema kuwa wanafanya shughuli hizo ili waweze kupata pesa ya kununua baadhi ya mahitaji yao ikiwemo madaftari pamoja na mavazi.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamewashauri wazazi kuwapatia watoto wao mahitaji ya msingi  ili  kuzuia kujiingiza katika makundi ya kihalifu.

Judith Mbukwa kutoka katika kitengo cha  dawati la jinsia mkoani Katavi  amewataka wananchi  ­­­­­­kutoa taarifa za wazazi waliotelekeza familia zao ili sheria ichukue nafasi kuwawajibisha.

Aidha Afande Judithi amewataka wazazi kuhudhuria Clinic ili kupatiwa ushauri kuhusu uzazi wa mpango ili wapate watoto watakaoweza kuwahudumia.