Mpanda FM

Wananchi Watema Cheche Kuhusu Vipodozi Vyenye Kemikali

04/10/2022, 5:32 AM

MPANDA

Baadhi ya Wananchi wa manispaa ya  mpanda mkoani katavi wametoa maoni yao kuhusiana na madhara yanayosababishwa na matumizi ya vipodozi vyenye kemikali.

Wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wamesema kuwa kuna  madhara kwa mtu anayejichubua anaharibu ngozi yake na anaweza kupata kansa ya ngozi.

Kwa upande wake Kaimu meneja shirika la viwango Tanzania TBS  ROBINI OBADIA Amesema kuwa kuna vipodozi vyenye viambata vya sumu vimezuiliwa kuingia nchini na vinasababisha madhara ya kiafya.

Serikari imekuwa ikichukua hatua ya kuviteketeza vipodozi vyenye viambata vya sumu na wakiendelea kuwapa elimu wafanyabishara.