Mpanda FM

Wananchi Walalamikia TOZO ya Taka

7 September 2022, 11:03 am

MAJENGO-MPANDA

Wananchi wa kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamelalamikia tozo ya taka kuwa kubwa na kusema kuwa hata utolewaji wa taka hizo ni wa kusuasua.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wengine Sarafina Paul amesema tozo ya taka inayotolewa ya shilingi 2000 kwa mwezi ni nyingi wanaomba wapunguziwe kwani hata ubebaji wa taka hizo haufanyiki kwa ufanisi.

.

Diwani wa kata hiyo Wilium Mbogo amesema kiasi hicho cha fedha cha shilingi 2000 inayotozwa kwa wananchi inasaidia katika kukamilisha uzolewaji wa taka hizo huku akikiri juu ya ucheleweshwaji wa kuondolewa kwa taka hizo kutokana na uhaba wa magari ya taka.

.

Diwani Mbogo amewaomba Wananchi kushirikiana vyema katika kuleta ufanisi wa kuyafanya mazingira kuwa safi kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha ili kufanikisha malengo.