Mpanda FM

Wananchi Wahoji Mil. 10 Kutumika Kujenga Choo Mnadani

7 September 2022, 10:55 am

KATAVI

Uongozi wa Kata ya Majengo Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi umetoa ufafanuzi  juu ya   swali la mwananchi kutaka kujua kiasi cha fedha cha Tsh Milion kumi kilichotumika katika ujenzi wa choo cha wafanyabiashara wa Mnada Kapripoiti.

Akizungumza katika Mkutano mara baada ya kusomwa kwa risala mmoja wa wananchi wa kata hiyo Yosesilaus Mapula amewataka viongozi kukagua choo hicho kwa  kulinganisha na kiasi cha fedha hiyo  ambacho kimetumika kujengea choo hicho.

.

Akijibia hoja hiyo diwani wa kata hiyo Wilium Mbogo amesema ujenzi wa majengo ya serikali unatofautiana na  ujenzi wa majengo  mengine na   unaenda kwa viwango hivyo hutumia gharama kubwa  .

.

Diwani Mbogo ameishukuru serikali kwa Kuwapatia choo katika eneo hilo la biashara ya Mnada na kusema kuwa mnada huo unawaongezea kipato wakazi wa kata hiyo.