Mpanda FM

Wananchi Wa Ivungwe Walilia Shule Shikizi

5 September 2022, 11:08 am

IVUNGWE

Wananchi wa Kitongoji cha Ivungwe A kijiji cha Kasokola wameulalamikia uongozi wa serikali ya kijiji kwa kushindwa kuendeleza Mpango wa kujenga shule shikizi katika kitongoji hicho licha ya kuchanga pesa na kufyatua tofali.

Wakizungumza na Mpanda radio fm wananchi wamesema ni muda mrefu umepita tangu wachangie pesa na kufyatua tofali kwa ajili ya kuanza ujenzi mpaka kuharibika kwa matofali ya ujenzi na kuitaka serikali ya kijiji kutoa mustakakabali wa ujenzi wa shule hiyo.

.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha kasokola Carlos Joackim Malufwa amesema mchakato wa kujenga shule utaendelea siku za karibuni kutokana na mvutano wa idadi ya wakazi wa Ivungwe kutatuliwa na kuwaomba wananchi kuendelea kuunga mkono  wakati shughuli za ujenzi zitakapoanza.

.

Kuanza kwa ujenzi huo kutafanikisha upatikanaji wa shule katika kitongoji cha Ivungwe ambapo kwa sasa watoto wamekuwa wakipata huduma ya elimu katika vitongoji vya jirani vya kasokola na luhafwe.