Mpanda FM

Kizungumkuti Viwatilifu Vya Korosho

05/09/2022, 10:51 AM

Wananchi wa kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda Halimashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamelalamikia kutopewa viwatilifu  kwaajili ya zao la korosho  licha ya kuwa wakulima wa zao hilo zaidi ya miaka mitano.

Wakizungumza na kituo hiki wakulima hao wamesema kuwa  wanapohoji juu ya viwatilifu hivyo wamekuwa wakipokea  kauli za  vitisho kutoka kwa viongozi

.

Hamis Rashid mbogo ambae ni mwenyekiti wa kijiji cha  Isinde amekiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi  na ameahidi kufuatilia suala hilo ili kuwapatia haki wakulima hao.

.

Mpanda radio imemtafuta Afisa kilimo  mkoani hapa faridi Mtiru ambapo amebainisha kuwa wakulima ambao hawajapata viwatilifu hivyo wafike katika ofisi za vijiji kwaajili ya kujindikisha ili waweze kupata katika awamu nyingine.

.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alikabidhi Jumla ya viwatilifu 921 kwa wakulima   wazao la korosho mkoani hapa kupitia  bodi ya korosho Tanzania.