Mpanda FM

WAZAZI SIMAMIENI MALEZI KUPUNGUZA WATOTO WA MITAANI

08/06/2022, 3:42 PM

Baadhi ya wazazi na walezi mkoani katavi wameshauriwa kuwalea watoto katika misingi bora ili kuepuka janga la watoto wa mitaani na mmomonyoko wa maadili.

Wakizungumza na mpanda fm baadhi ya wazazi hao wamesema kuwa hali duni ya maisha ndio sababu ya ongezeko la watoto wa mitaani na mmomonyoko wa maadili kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kukidhi mahitaji ya mtoto.

Kwa upande wake Kelvin Fuime kutoka jeshi la polisi mkoa wa katavi kitengo cha dawati la jinsia na watoto amesema kuwa malezi ya mabovu ya baadhi ya wazazi ndio chanzo cha watoto wa mitaani hivyo ameitajka jamii kuzingatia katika malezi ya watoto.

Kila ifikapo june 1 kila mwaka dunia huadhimisha siku ya wazazi huku lengo ni kukumbusha wajibu wa mzazi na mlezi katika kuilea familia katika misingi iliyo bora.