Mpanda FM

WANANCHI WALALAMIKIA VIBAO VYA MBAO

8 June 2022, 4:17 pm

MPANDA

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa mtemibeda  kata ya misunkumilo manispaa ya  mpanda mkoani katavi wameutaka uongozi wa manispaa kuondoa vibao vya mbao vinavyoonesha majina ya mitaa na barabara na badara yake kuwekewa vya chuma  kama ilivyo kwa  maeneo mengine.

Wakizungumza na mpanda redio fm wananchi hao  wamesema kuwa bado wamejiuliza kwanini manispaa imepeleka vibao vya mbao vinavyoonesha majina ya mitaa na barabara katika mtaa huo na sio vibao vya chuma kama ambavyo serikali imeeagiza.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata ya misunkumilo  Mussa Kiteka  amekili kupokea vibao hivyo vya mbao kutoka manispaa na kupewa maagizo  ya kuviandika majina na kuvibandika katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo.

Zoezi la anuani za makazi linaendelea kufanyika mkoani katavi kwa kuendelea kubandika namba za makazi kwa kila nyumba  na vibao vinavyoelekeza majina ya mitaa na barabara.