Mpanda FM

WANANCHI WAASWA KUJIKINGA NA BARIDI KUTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

8 June 2022, 4:19 pm

Wananchi mkoani katavi wametakiwa kuchukua tahadhali ya kujikinga na baridi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika kipindi cha mwezi june hadi agosti.

Hayo yamebainishwa na Emily Elinest  kutoka mamlaka ya hali ya hewa Tanzania mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa kuwango cha joto kina tarajiwa kuwa nyuzi joto 14 hadi 20 mkoani Katavi ambapo tofauti na msimu mingine iliyopita.

Aidha Elinest amewataka wananchi kufatilia kwa ukaribu taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na mamlaka hiyo na kuchukua tahadhali .

Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania ilitangaza mwelekeo wa kipupwe unaotarajiwa kuanza juni hadi agosti mwaka huu katika mikoa mitano ya kanda ya nyanda za juu kusini magharibi yenye miinuko inatarajiwa kuwa na baridi kali chini ya nyuzi joto 4.