Mpanda FM

WAMILIKI WA MAGHALA WAASWA KUTUNZA NYARAKA KUSAIDIA KUPATA TAKWIMU ZA UZALISHAJI WA CHAKULA

8 June 2022, 4:09 pm

Afisa kilimo manispaa ya Mpanda Benatus Ngoda  amewataka Wamiliki wa maghala ya kutunzia vyakula mkoani Katavi kutunza nyaraka ili kusaidia kupata takwimu sahihi za chakula kinachozalishwa kwa mwaka nchini na kutunza chakula kwa usalama.

Akizungumza na Mpanda radio fm Ameeleza tofauti na kujua takwimu za kilimo kwa mwaka pia utunzaji wa nyaraka una mchango kujua uchumi wa mkulima unaongezeka kiasi gani kutokana na utunzaji kumbukukumbu kuwezesha mkulima kujipa nafasi ya kufanya tathmini.

Kwa upande wake afisa kilimo kata ya kakese Abel Bonifas nzowe amesema kuwa  jamii ya wakulima bado inamuamko  mdogo wa kujenga maghala ya kuhifadhia chakula huku akitoa  wito kwa wakulima kujenga maghala hayo  ili kusaidia wakati wa kutunza chakula na kurahisisha utafutaji wa takwimu za mazao.

Wataalamu wa  kilimo wameainisha faida za kuhifadhi mazao kwenye ghala ikiwa  ni kusaidia kuhifadhi takwimu, kusaidia  pia kuunganishwa na wateja   .