Mpanda FM

WAKULIMA WA MPUNGA WAASWA KUTUMIA NJIA ZA KISASA KUHIFADHI MAZAO

8 June 2022, 3:55 pm

Wakulima wa Mpunga mkoani Katavi wameaswa kutumia njia za kisasa za kuhifadhi zao hilo mara baada ya kuvuna ili waweze kuendana na utunzaji bora kwa manufaa ya  zao hilo likiingia sokoni.

Akizungumza na Mpanda radio fm afisa kilimo kata ya Kakese Abel bonifasi Nzoye ameainisha  faida za kuhifadhi zao hilo ni kuunganishwa na wanunuzi moja kwa moja  huku akiwasihi  kuacha kuhifadhi mazao majumbani  kwa kigezo cha kupunguza gharama za kuhifadhi kwenye ghala maalumu.

Nyiti Salu Kulwa mkulima na  mmiliki wa ghala la kuhifadhia chakula lililopo kijiji cha mbugani kata ya kakese amesema kuwa Amekuwa akiwapa elimu wakulima jinsi ya kutunza mpunga ili usiweze haribika kutokana madhara ambayo ambayo yalishamtokea katika kilimo chake.

Kwa mijibu wa afisa kilimo kata ya kakese wakulima mkoani hapa w zao la mpunga bado wanalima kimazoea na si biashara.