Mpanda FM

MADARASA NA MADAWATI BADO CHANGAMOTO KATA YA KASOKOLA

08/06/2022, 3:41 PM

Kata ya kasokola iliyopo manispaa ya mpanda inakabiliwa na upungufu wa miundo mbinu wa madarasa na madawati katika shule za msingi na sekondari.

akizungumza  na Mpanda radio fm katika kipindi Cha kumekucha Tanzania Diwani wa kasokola  Crisant  Andrea Mwanawima amesema kuwa shule ya sekondari inakabiliwa na upungufu wa madawati 82 na upande wa shule ya msingi ikikabiliwa na uhaba wa madarasa.

Katika hatua nyingine Mwanawima ameiomba serikali katika ajira zilizotangazwa za walimu kuwapatia walimu ili kuweza kuinua ufaulu wa shule za msingi na sekondari katika kata hiyo.

Kwa mujibu wa diwani huyo mkoa wa katavi umekuwa na changamoto katika sekta ya elimu upande wa  miundombinu pamoja na uchache wa waalimu Hali inayopelekea kutokupanda kielimu .