Mpanda FM

UMASKINI, CHANZO MIMBA ZA UTOTONI

23 May 2022, 1:42 pm

KATAVI

Umaskini wa kipato umetajwa Kuwa  chanzo moja wapo  cha kinachopelekea mimba  za utotoni  kwa baadhi ya familia mkoani katavi.

Wakizungumza na mpanda redio fm baadhi ya wazazi hao  wameeleza namna umaskini wa familia unavyosababisha mabinti wengi kupata mimba kabla ya umri, kuwa ni kutopata mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi  na walezi wanaoishi nao.

Kwa upande wake mratibu wa polisi jamii na dawati la jinsia na watoto mkoa wa katavi inspekta Kelvin Fuime amesema watoto wa kike wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye mahusiano kwa lengo la kujitafutia mahitaji binafsi ambayo wanayakosa nyumbani.

Mkoa wa katavi ni miongoni  mwa mikoa ambayo inaongoza  kwa mimba za utotoni  ambapo kitaifa inashika nafasi ya kwanza .