Mpanda FM

MIL. 470 KUWANUFAISHA SHULE MAALUM MSAKILA

23/05/2022, 2:34 PM

Jumla ya shilingi million 470 zimetolewa katika wilaya ya Tanganyika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya msingi   katika shule maalumu ya msakila.

Akizungumza na Mpanda radio fm kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Tanganyika Betuel Luhega wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya Ya Tanganyika   Onesmo Buswelo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule  amesema kuwa pesa  zitatumika kadiri zilivoelekezwa kupata miundombinu bora.

Nae mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelo amemtaka mkurugenzi kutobweteka kuendelea kusimamia kwa umakini mradi huo huku akisisitiza kushirikishwa  kwa taasisi nyingine ili kuweka mindombinu bora katika shule hiyo.

Mpaka sasa ujenzi unaoendelea ni mabaara tatu, madarasa nane, jengo moja la utawala, matundu kumi ya vyoo maktaba pamoja na chumba cha Tehama.