Mpanda FM

MIGOGORO WAKULIMA NA WAFUGAJI HALI TETE

23/05/2022, 1:56 PM

KATAVI.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Karema  mkoani katavi wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro   kati ya wakulima na wafugaji kabla haujaleta madhara makubwa katika  jamii.

Wakulima hao wameiambia mpanda radio fm kuwa ugomvi kati ya wafugaji na wakulima umekuwa ukitokea mara kwa mara ndani ya kijiji hicho na kusababisha shughuli za kilimo kutofanyika  ipasavyo.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kijiji hicho wameeleza namna ambavyo walivyopigwa na wafugaji   wakati wakiwa katika majukumu yao ya utekelezaji wa kulinda mazao ya wananchi ambayo  yanaharibiwa na mifugo.

Hali hiyo ikampelekea Mkuu wa wilaya ya tanganyika onesmo buswelu kuliagiza  jeshi la polisi wilayani humo kumukamata  mfugaji ajulikanae kwa jina Runyalaja Omari na wenzake wanaodaiwa kufanya fujo ikiwemo kuwapiga  viongozi wa kijiji cha Karema  wakati wakitekeleza majukumu yao wilayani Tanganyika.

Migogoro kati ya wafugaji na wakulima wilayani humo imekuwa ikiripotiwa mara kadhaa huku chanzo kikubwa kikitajwa kuwa ni wafugaji kuingia kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima .