Mpanda FM

RADI YAUWA NG’OMBE 28 KATAVI

30 March 2022, 4:29 pm

KATAVI

Ng’ombe 28 kati ya 52 waliokuwa pamoja wanatoka malishoni wa kaya tano tofauti kijiji cha Kabage kata ya Sibwesa Wilayani Tanganyika mkoa wa katavi zimekufa baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua na upepo mkali.

Hayo yameelezwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Ally Makame Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuwataja wamiliki wa ng’ombe hao.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Ally Makame akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Sauti ya kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa katavi ACP Ally Makame Hamad

Aidha ACP Makame ameeleza kuwa baada ya tukio hilo wanakijiji hao walijumuika kwa pamoja kufanya kisomo ili Mungu awaepushe na madhara ya majanga kama hayo.

Sauti ya Kamanda Makame

Matukio ya mifugo kufa kwa radi yamekua yakijirudiarudia mara kwa mara katika msimu huu wa masika ambapo march 08 mkoani manyara ng’ombe 16 na mbuzi 5 walikufa kwa radi.