Mpanda FM

TRA Mpanda Yakusanya Mil. 371 kwa Mwezi

20/11/2021, 10:32 AM

Mamlaka ya mapato wilaya ya  mpanda Mkoani katavi  imefanikiwa kukusanya shilingi milioni mia tatu sabini na moja kwa kipindi cha mwezi augusti sawa na asilimia themanini na tisa ya lengo lililopangwa.

Kauli hiyo imetolewa na afisa kodi daraja la kwanza Mashenene Benny na kusema lengo ilikuwa ni kukusanya shilingi milioni mia nne kumi na sita ndani ya mwezi augusti ila wameshindwa kufikia lengo kufatia kampuni ya katavi mining kushindwa kulipa milioni mia mbili arobaini na sita.

Aidha mashenene amefafanua juu ya tozo ya majengo inayolipwa kwa njia ya luku nakusema wale wote ambao walikatwa kodi hiyo kimakosa watarudishiwa pesa zao kwa njia ya tokeni za umeme.

Tozo ya majengo kupitia malipo ya umeme kwa njia ya luku ilianza mwezi wa saba mwaka huu baada ya tamko kutolewa na waziri wa fedha na mipango dokta Mwigulu Nchemba.