Mpanda FM

Mifumo Mibovu ya Maisha Chanzo cha Magonjwa Yasiyoambukiza

20/11/2021, 10:44 AM

Wananchi mkoani katavi wameshauliwa kubadili mtindo wa maisha ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo.

Kauli hiyo imetolewa na daktari wa idara ya magonjwa yasiyoambukiza kutoka  hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi dokta  Daniford Mbohilu akifanya mahojiano na mpanda redio fm na kusema matatizo ya moyo husababishwa na mtindo wa maisha ambao watu wanaishi bila kuzingatia utaratibu wa kiafya.

Sauti ya Dr. Danford

Aidha Mbohilu amewataka watu kuishi maisha yenye afya na kuwa na tabia ya kuchunguza afya  mara kwa mara, pia kuzingatia ufanyaji wa mazoezi ili kupunguza uzito uliozidi mwilini.

Sauti ya Dr. Danford akitoa ushauri

Kila ifikapo tarehe ishirini na tisa ya mwezi  wa tisa kila mwaka dunia huazimisha siku ya moyo.