Mpanda FM

Mabalozi Wapewa Darasa na Ewura

20/11/2021, 1:13 PM

Mwenyekiti wa baraza la ushauri watumiaji wa huduma za nishati na maji katika mkoa wa Katavi EWURA CCC Steven Kinyoto amewataka wenyeviti wa mitaa katika manispaa ya Mpanda kuwa mabalozi kwa kuelimisha jamii katika kupata haki zao kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji

Wito huo ameutoa katika semina iliyoshirikisha viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa serikali katika manispaa ya Mpanda ambapo ameleeza kuwa kufanya hivyo kunakwenda kusaidia jamii kutambua namna ya kudai haki yake pindi anapokuwa na changamoto ya huduma katika utumiaji wa nishaji na maji

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa katika manispaa ya Mpanda wameshukuru elimu hiyo waliopatiwa na kuahidi kuwa watakwenda kuelimisha jamii inayowazunguka kufahamu namna ya kuweza kupata msaada pindi unapokubwa na changamoto ya katika utumiaji wa nishati na maji

Semina hiyo iliyoandaliwa na baraza la ushauri watumiaji wa huduma za nishati na maji katika mkoa wa Katavi EWURA CCC  kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa ili kutambua haki na wajibu ya kusimamia na kutatua haki za watumiaji wa nishati na maji.