Mpanda FM

Wanawake Acheni Kukanda Maji

19/11/2021, 11:16 AM

Wanawake mkoani Katavi wametakiwa kuachana na dhana ya kuwakanda  maji ya moto pindi wanapojifungua  kwani kufanya hivyo kuna madhara zaidi ikilinganishwa na faida zinazoainishwa na jamii nyingi.

Editha Ngavatula ni muuguzi katika hospitali teule ya mkoa wa Katavi amesema kuwa kukandwa kunaweza msababishia mwanamke kupata maumivu makali,kuharibu maumbile na kulegeza misuli.

Sauti ya Muuguzi

Mpanda radio fm imezungumza na baadhi ya wanawake ambapo wameeleza kuwa kukandwa maji moto huwasaidia kupona kwa haraka baada ya kujifungua na kuondoa uchafu uliosalia tumboni.

Sauti ya Wanawake

Mnamo mwaka 2019 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama, wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imesema kuwa mtindo wa kuwakanda na maji ya moto wanawake wakishajifungua ni hatari.