Mpanda FM

Mpanda Hotel Kuimarisha Ulinzi

19/11/2021, 10:58 AM

Wananchi wa mtaa wa mpanda hotel manispaa ya mpanda mkoani katavi wameuomba uongozi wa mtaa huo kuimarisha ulinzi na usalama ili kudhibiti changamoto itokanayo na vikundi vya uhalifu katika mtaa huo.

Wakizungumza na mpanda fm kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya vijana kushiriki katika vitendo vya uhalifu wakati wa usiku hususani uvunjifu wa milango katika nyumba za watu.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mpanda hotel Christina abdulaham amesema kuwa kila mwananchi  anao wajibu wa kuendelea kulinda mali zake kutokana wao kuto kukubaliana katika suala la kuchanga michango kwa ajili ya kuwalipa wanao fanya uliNzi nyakati za usiku.

Sauti ya Mwenyekiti

Mbali na hayo mwenyekiti huyo ameendelea kuwaasa wananchi wa mtaa huo kutambua kuwa kila mmoja anao wajibu wa kulinda mali zake sambamba na kuepuka kujingiza katika vitendo vya uhalifu.