Mpanda FM

Katavi na Maadhimisho ya Magonjwa Yasiyoambukiza

19 November 2021, 12:01 pm

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza wameeleza  umuhimu wa mazoezi sambamba na kuwaasa wananchi wenzao kujitokeza kwenye mazoezi.

Wameyasema hayo walipozungumza na mpanda redio fm katika uwanja wa Azimio ambapo yaefanyika maadhimisho ya wiki ya kilele cha wiki ya magonjwa yasiyo ambukiza leo 13/11/2021

Sauti za Wananchi

Aidha Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza Mkoani Katavi Mohammed Mbunjo amesema kuwa dhumuni la maadhimisho hayo ni kuwapa wananchi uelewa pamoja na kutambua kuwa magonjwa yasiyoambukiza yameongezeka.

Sauti ya Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza Katavi

Ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza inashauriwa kuzingatia lishe bora, kuepuka unywaji wa pombe, matumizi ya sigara na madawa ya kulevya, kufanya mazoezi na kupata muda mzuri wa kupumzika.