Mpanda FM

Bilioni Nne Kunufaisha Halmashauri ya Nsimbo

19/11/2021, 10:29 AM

Halmashauri ya  Nsimbo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imepata zaidi ya shiling bilioni nne kwa ajili  ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo vyumba vya madarasa.

Akizungumza na kituo hiki mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed Ramadhani amesema kuwa  kupatikana fedha hizo ni neema kubwa kwa halmashauri hiyo kwani itasaidia   kupunguza baadhi ya changamoto  ikiwemo  kuongezeka kwa vyumba vya madarasa

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri Nsimbo

Aidha Ramadhani amewataka wananchi katika halmashauri hiyo kuendelea kuziunga mkono  kwa vitendo juhudi zinazoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa  kuwa walinzi  juu ya watu wenye lengo baya juu ya miradi hiyo

Halmashauri ya nsimbo ni miongoni  mwa Halmashauri za manispaa ya mpanda mkoani katavi zilizo pokea fedha zaidi ya bilioni nne  zilizotolewa na serikali kutoka benki ya dunia