Mpanda FM

12,000 Wapata Chanjo ya Sinopharm

19/11/2021, 10:14 AM

KATAVI

Zaidi ya wananchi elfu nne mkaoni katavi wamepata chanjo  ya dozi ya kwanza ya  sinopharm na kufanya idadi ya watu waliopata chanjo ya uviko19 kufikia elfu kumi  na mbili mkoani hapa.

Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa mkoa wa katavi dr omari sukari wakati akizungumza na kituo hiki ambapo ameeleza  huduma mkoba imerahisisha kuwafikia wananchi wengi kupata chanjo.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi

Aidha  baadhi ya viongizi wa dini ,taasisi zisizo za kiserikali na wadau mbalimbali wamethibitisha kutokupata madhara yoyote baada yakupata chanjo ya uviko19.

Sauti za Wadau mbalimbali

Tarehe 4 mwezi wa nane mkoa wa katavi ulizindua huduma ya mpango shirikishi wenye lengo la kuwafikia wananchi wengi kupata chanjo ya uviko -19 kwa urahisi .