Mpanda FM

Mufti Mkuu Tanzania: Bakwata tafuteni hati

13/10/2021, 8:58 AM

  • OKTOBA 6, 2021

KATAVI

Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zuberi amewataka makatibu wa misikiti yote Mkoani katavi kuhakikisha wanapata hati miliki za viwanja vyote vinavyomilikiwa na baraza la waislam Tanzania BAKWATA.

Shekh mkuu wa Tanzania ameyasema hayo alipotembelea shamba la mikorosho  linalomilikiwa na baraza hilo mkoani hapa na kueleza kuwa ili kuondokana na  migogoro ya ardhi ni vyema ardhi hizo zikapatiwa hati miliki.

Akitoa taarifa ya shamba hilo katibu wa msikiti wa madina Khalid  Chibila  amesema kuwa shamba hilo la mkororosho linathamani ya shilingi Milioni Moja na Laki Tatu huku akibainisha kuwa mpaka ifikapo 2023 wanatarajia  kuvuna korosho katika shamba hilo.

Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zuberi akizindua mradi wa shamba la korosho unaomilikiwa na Bakwata mkoani Katavi.

 Muft na Shekh mkuu wa Tanzania  yupo mkoani katavi kwa ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi mbalimbli ya baraza kuu la waislam Tanzania.