Mkoani FM

Vipindi  vya elimu Redioni vitaengeza ufaulu Sekondari.

14 September 2023, 3:58 pm

Meneja wa mradi wa  Secondary  Radio Education ( SRE)   Jun sug an  Baraka (Picha na Said Omar)

Vipindi vya elimu vya redio zinasaidia kuengeza ufauli kwa wanafunzi hasa wa sekondari ni vyema wazazi na walimu kushirikiana kwa pamoja kuwahimiza watoto wao  kufuatilia vipindi hivyo kwa lengo la kuengeza ufaulu.

Na Fatma Rashid.

Meneja wa mradi wa  Secondary  Radio Education ( SRE)   Jun sug an  Baraka amewataka  wazazi  na walimu kuwahamasisha wanafunzi wa sekondari kujifunza kupitia vipindi vya  redio  kwa lengo la kukuza ufaulu wao.

Ameyasema hayo katika ghafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha elimu kupitia vipindi vya redio Pemba iliyofanyika  katika ukumbi wa Chuo cha SAMAIL Gombani Chake Chake Pemba.

Pia amesema kuwa Elimu ndio njia pekee ya kubadilisha maisha hivyo amewataka wazazi na walimu  kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuwashawishi wanafunzi  kujifunza kupitia redio kwani itasadia kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Meneja wa mradi wa  Secondary  Radio Education ( SRE)   Jun sug an  Baraka

Akizungumza  Afisa Elimu Mkoa wa Kusini Pemba Mohammed Shamte kwa niaba ya Mgeni Rasmi Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu Pemba Mohammed Nassor Salim  amewashukuru KOICA na good Neighbours kwa yote waliyoyafanya katika Elimu kwani ni mambo yenye tija kwa Wizara na wanafunzi.

Hata hivyo amesema kuwa  Redio ndio nyenzo muhimu sana kwa kuwahamasisha wanafunzi kuweza  kujifunza na kufaulu vizuri katika masomo yao  hivyo wazazi na walimu wana jukumu lao kuwasimamia watoto kujifunza.

Afisa Elimu Mkoa wa Kusini Pemba Mohammed Shamte

Kwa upande wake mtoa mada ya Wazazi kusimamia watoto wao kwenye elimu   Ndugu,Sabrina Ali Batashi amewasisitiza wazazi kuwashawishi watoto wao kujifunza kupitia vipindi vya redio  kwani watajifunza vitu vingi vitakavowasaidia  kufanya vizuri katika masomo yao

Pia amesema kuwa mzazi ndie mtatuzi  mkubwa wa kutatua changamoto za mtoto na kumsaidia kuleta mabadiliko 

Kwa upande wa washiriki katika ghafla hiyo wamesema kuwa ni jukumu la wazazi kuwalea watoto wote  katika jamii zao kama watoto wao na kusiwe na mtu na mwanawe tu kwani jamii ili iendelee ni lazima wazazi waungane kuwalea watoto wao.

Mradi huo wa miaka bmiwili  unaotekelezwa na  GOOD NEGHBOURS  kwa kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanziabar kwa ufadhili  wa shirika  la ushirikiano la kitaifa  korea KOICA  kwa lengo la kukuza ufaulu wa Wanafunzi Sekondari wa Zanzibar   kwa njia ya kujifunza kupitia vipindi vya Redio.

Kufuatia kifo cha aliyekuwa  Mwakilishi wa jimbo la mtambwe, tume ya uchaguzi  Zanzibar imeamua kufanya uchaguzi mdogo kuziba nafasi hiyo iliopo wazi na wadau wote wa uchaguzi wanatakiwa kushiriki kukamilisha uchaguzi huo kama ilivyokusudiwa.