

9 September 2023, 2:28 pm
Prf, Mnyaa Mbarawa akitekeleza ahadi yake ya kuwajengea skuli wananchi wa sheia ya Chokocho ambapo kwa sasa eneo hilo kuna skuli moja tu ambayo wanasoma wanafunzi wa sekondari na Msingi wakiingia kwa nyakati za asubuhi na mchana .
Na Khatib Nahoda.
Jumla ya shilingi Milioni 50 zinatarajiwa kutumika katika hatua ya mwanzo ya ujenzi wa mabanda ya kusomea ya skuli ya chokocho wilaya ya mkoani mkoa wa kusini Pemba.
Akizungumza mara maada ya kukabidhi vifaa vya ujezi wa mabanda nane kwa kamati ya skuli hio katibu wa mbunge wa jimbo mkoani Mariam Said Khamis kwa niaba ya Mbunge wa jimbo hilo Profesa Makame Mbarawa amewataka wanachi wa wajimbo hilo kuunga mkoano juhudi za kimaendeleo zinazo fanywa na mbunge wao kwa lengo kuleta maendeleo.
Amesema kwa niabaya mbunge huyo ata hakikisha ujenzi huo uliopo hatua ya awali unakamilika na hatua ya pili ili kuondosha changamoto ya uhaba wa vyumba vya kusomea.
Sambamba na hayo amewataka wananchi wa shehia hio ya chokocho kutoa ushirikiano kwa amafundi na kuhakikisha wanakua walinzi wa vifaa vilivyotolewa ili lengo la ujenzi litimie kama ilivyokusudiwa.
Nae mwenye kiti wa CCM jimbo la mkoani Omar Ngwali Dadi amesema kutolewa kwa vifaa hivyo ni utekelezaji wa ilani ya chama na utekelezaji wa ahadi alizoziweka mbunge huyo.
Idi Abdala Idi mwenye kiti wa kamati ya skuli ya chokocho sekondari amesema mabanda hayo yatakapo kamilika yataondosha changamoto walioyonayo kwa muda mrefu pia ufaulu wanafunzi utaongezeka.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa skuli ya sekondari chokocho Haji Shoka amesema ujenzi huo wenye vyumba nane vya kusomea , maabara, chumba cha komputa, ofisi za walimu pamoja na vyoo utakapo kamilika utatoa ufanisi wa ufundishaji kwa walimu na kuongeza kiwangocha ufaulu.
Amesema kwa sasa skuli hiyo ina mchanganyiko kwa wanafunzi wa sekondari na msingi kwa kuwakosesa wanafunzi utulivu wa kosoma na kupelekea matokeo yao kutokua mazuri kama inavyotarajiwa.
Vifaa vilivyo kabidhiwa kwahatua ya awali katika skuli ya chokocho ni mawe, matofali,kokoto , nondo, mchanga pamoja na suruji pakti 300.