Mkoani FM

Mtu mmoja ajeruhiwa na watu wasiojuilikana Pemba

8 September 2023, 12:02 pm

Ndugu Machano Ali Ame ambae amejeruhiwa na watu wasiojuuilikanana akiwa kwenye kambini ya Karafuu shehia ya chumbageni Wambaa(Mwaandishi Wetu)

Mmiliki wa kambi ya uchumaji  zao la karafuu anajeruhia na watu wasiojuuilikana huko kambini kwake  matukio hayo yanajitokeza kila msimu wa karafuu unapofika  kisiwani Pemba.

Na Mwandishi wetu.

WATU wasiofahamika Wadaiwa kuvamia kambi ya karafuu na Kumshambulia kwa vitu vyenye ncha kali mmiliki wa kambi hiyo Machano Ali Ame mkaazi wa Bumbwini Misufini wilaya ya Kaskazini B Unguja tukio lilitokea juzi majira ya saa 5 usiku huko Chumbageni wambaa wilaya ya Mkoani mkoa wa Kusini Pemba

Akisimulia jinsi alivyokutwa na mkasa huo  Majeruhi huyo  akiwa katika hospital ya Abdalla Mzee kwajili ya matibabu  amesema  watu  hao waliomvamia katika kambi hiyo huku akiwa usingizini jambo ambalo lilipekea kutokuwafahamu watu hao waliomshambulia  kwa vile alishutuka  na kupiga mayowe kwajili ya kutaka msaada wa kunusuru uhai wake.

Ndugu Machano Ali Ame mbae amejeruhiwa.

Akithibitisha  kupokea  Majeruhi huyo  Daktari dhamana hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Rashid  Saleh Hemed  amesema hali ya majeruhi huyo kwa sasa inaendelea vizuri ambapo  mnamo saa sita usiku alifikishwa hospitalini hapo  akiwa na majeraha mbali mbali   ikiwemo sehemu za kichwa pamoja na mabega.

Daktari dhamana hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Rashid  Saleh

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Siprian Alaice Mushi amekiri kupokea taarifa hizo ambapo amesema jeshi la polisi linaendelea  na uchunguzi zaidi .

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Siprian Alaice Mushi