Mkoani FM

WAKULIMA WA MPUNGA WAMPA KONGOLE BI MAIBA AFISA UMWAGILIAJI.

17 March 2023, 2:44 pm

Na Amina Massoud Jabir

Wakulima wa mpunga wa umwagiliaji bonde la Kindani na Machigini wilaya ya mkoani pemba wamepongeza juhudi zinazichokuliwa na kiongozi mwanamke katika kuwasimamia namna bora ya uzalisahji wa mazo yao.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wakulima Issa Khamis, Amina Haji na  Raya Omar wamesema, hapo awali kulikua na ungumu wa ufuatiliaji changamoto zinazowakabili wakulima lakini kufuatia kuwepo kwa afisa msimamizi mpya ambae ni mwanamke kumesaidia kutatua changamot kwa haraka na kwa wakati hitajika.

Wameongeza kuwa kupitia juhudi hizo wameongoeza uzalishaji ukilinganisha na hapo awali, na kuwataka wakulima wenzao kuunga mkono juhudi hizo.

Afisa umwagiliaji Wilaya ya Mkoani Maiba Mussa Skuni amesema wanaendelea kuwapatia elimu juu ya umuhimu wa kufuata utabiri wa hali ya hewa kabla ya kuanza kulimo sambamba na kuzalisha mbolea za asili ili kuongeza kiwango cha uzajilishaji wa kilimo cha aina hiyo.

Kisiwa cha Pemba kinajumla ya mashamba ya umwagiliaji 12 huku Wilaya ya Mkoani ikiwa na mashamba 3 yakiwemo ya Darajani Kindani na Machigini.