Mkoani FM

MAJI YA UHAKIKA KUBORESHA ELIMU MAKANGALE KUPITIA DC YA MICHEWENI.

17 March 2023, 2:24 pm

Na Khadija Rashid Nassor.

Kupatikana kwa maji safi na salama katika Skuli ya Mnarani msingi kuewezesha wanafunzi wa skuli hiyo hususan wanawake kuhudhuria masomo yao ipasavyo.

Wakizungumza wanafunzi Maryam Said na Ali Hassan wamesema hapo awali walilazimika kutembea masafa ya mbali kufuata huduma hiyo hali iliyopelekea kukosa baadhi ya vipindi kutokana na kuchelewa kufika skuli kwa wakati husika.

Wameongeza  kua kutokana na ukosefu wa huduma hiyo ilipelekea kukaa bila kujisaidia kwa muda wote wanapokua skuli hali iliyokua ikichangia kutoroka au kutohudhuria skuli ipasavyo.

“ hatua ya mkuu wa wilaya Mgeni imetusaidia sana wanafunzi kwani tunapata muda nzuri wa kujisomea”

Salama Omar na Ali Mohammed wamesema kupatikana kwa maji skulini hapo kumewapa faraja hata wao wazazi kwani watoto wamekua wakisumbuka kwa muda mrefu na kutofikia ufanisi wa masomo yao.

“ tulikua hatuna lakufanya ila kama wazazi ilituuma watoto kukosa huduma hiyo skuli kwani masaa wanayokuwa huko sio kidogo na wengine ni watoto wadogo”

Mohd Sabri muuza maji ambae anapeleka maji skulini hapo akifafanua hali halisi ya upatikanaji wa maji shehiya ya Makangale amesema amelazimika kushirikina na MH. MGENI Khtibu Yahya kutokana na ukosefu wa maji uliodumu kwa miaka kadhaa.

 “ Ingawa ni mfanya biashara ila nimeona ipo haja yakushirikiana na Mh. Mgeni kupeleka maji kwa kila siku kijiji kimoj na kwa sasa nahudumia vijiji vinne”

 Suleiman kombo Ali Meneja Operasheni kutoka  KWANINI FOUNDATION iliopo Makangale amesema baada ya kupokea changamoto hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mgeni Khatib  kama jumuiya wameona ipo haja kuungana pamoja lengo ni kuchochea maendeleo Wilaya ya Micheweni.

“ Mi niwombe viongozi wanaochagulia au kuteuliwa  kufuata nyanyo za Mkuu  wa Wilaya ya micheweni  kwani amekua akishuka hadi katika ngazi za jamii kusikiliza changamoto na kuzitafutia ufumbuzi jambo linaloashiria uwepo wa UtawalaBora”.

Jumla ya vijiji vinne shehiya ya Makangale vlivyokuwa na changamoto ya maji kwa sasa vimeweza kufikiwa na kupatiwa huduma ya maji.