Mkoani FM

CHANAGAMOTO YA HEDHI SALAMA KWA WANAFUNZI WAKIKE YAPATIWA SULUHISHO.

2 January 2023, 1:45 pm

Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim, anasema, wizara imekuwa ikichukuwa juhudi ya kupambana na hedhi salama kwa wanafunzi wakike , kwa kuwapa elimu ya stadi za maisha ‘ABC’ .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ameeleza kuwa stadi za maisha hizo ni pamoja na kujitambuwa na udhalilishaji, kuwa salama na hedhi na kuimarisha miundo mbinu hususan yyoo sambamba na kuwepo waalimu wa kutosha wa ushauri nasaha wa msingi na sekondari.

Amesema  wakati mwengine hupata misaada ambapo hivi sasa wanazo Pedi 3000 ambazo watazigawa kwa wanafunzi walioko katika dakhalia (mabweni) kwa wanafunzi wastani wa 314 kisiwani Pemba pekee.

Ofisa ushauri nasaha wa kujitegemea kisiwani Pemba Sabahi Mussa Said anasema,  wamekuwa mstari wa mbele kutowa ushauri nasaha pale wanapokutana na wanafunzi ili kukabiliana na hali hiyo.

Mkurugenzi wa mradi wa kuwajengea  uwezo walimu katika mazingira rafiki ya moto wa kike) unaofadhiliwa na Korea (KHFI) Esther Mwakarobo ameeleza lengo la mradi huo, ni kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi hasa wa kike ili kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza, wakati wakiwa katika kipindi cha Hedhi.

Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Shumba Vyamboni Khatib Rashid Mwinyi  na mwalimu mkuu wa skuli ya sekondari Chwaka Tumbe Hamad Dadi Khamis,wameeleza  katika Skuli yako matatizo ambayo  yanawakabili watoto wa kike hasa pale wanapokuwa katika hedhi.

Kwa upande wao wanafunzi wamasema  wamekuwa wakipatiwa ushauri nasaha kutoka Skuli na hivyo umewasaidia sana na wamekuwa wakihudhuria madarasani kama kawaida ingawaje kuna changamoto wanazokumbana nazo baadhi ya wanafunzi ikiwemo kuumwa na tumbo.

mradi huo wa KFHI unaofadhiliwa na KOICA na kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  anaeleza kuwa mradi huoutakuwa ni wa miaka (3) na utatoa elimu kwa wanafunzi wapatao 1,300 na walimu 100 kwa Skuli tano (5).