Mkoani FM

Wananchi washauriwa kuunga mkono bishaa za wajasiliamali wa ndani

3 December 2022, 12:47 pm

HABIBA KHAMIS MOHAMMED MJASIRIAMALI WA UTENGENEZAJI WA UNGA WA HOPECA.

Wananchi kisiwani pemba wametakiwa kutumia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanawake ili kuunga mkono juhudi za kujikwamua na umasikini.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Habiba Khamis Mohd mjasiriamali na muuzaji wa unga wa lishe wa Hopeca amesema imefika wakati sasa kwa wanawake kujikwamua kwa kuanzisha vikundi vyao wenyewe.

Amesema ameamua kujiingza katika uuzaji wa unga wa lishe kwani ni chakula cha kuanzia siku pia dawa ya magonjwa mbalimbali yakiwemo pressure,vidonda vya tumbo, maumivu ya mgongi, kisukari, afya ya uzazi, afya ya ubongo, kukaukwa na damu, maradhi ya mifupapamoja na  homa ya mnjano.

UNGA WA HOPECA.

Kwa upande wa watmiaji wa unga  wa Hopeca  Ish-ra Mohd Juma na Fahmi Khamis Ali wamesema umeweza kuwasaidia  kuwaondoshea matatizo waliyokuwa nayo ukilnganisha na hapo awali.

2022 ameanza biashara yake na uuzaji wa unga wa hopecaa ambao ni unga ulochanganywa na mbegu tofauti zikiwemo mbegu boga, parachichi, tende, zaabibu, lozi na karanga.