Mkoani FM

Wahitimu kidato cha nne waaswa kujiendeleza kimasomo

28 November 2022, 7:50 am

Mratib wa kitengo cha elimu ya watu wazima Pemba Salim Kuza Sheikhan

WANAFUNZI waliomaliza mitihani ya kidato cha nne wametakiwa kujiwekea malengo ya kitaaluma maraa baada ya kumaliza elimu yoa ya lazima sambamba na kuwa na mashirikiano na wazazi wao ili kujanga jamii iliyo bora.

Akizungmza na wazazi na wanafunzi katika ghafla ya kuwaanga wanafunzi waliomaliza mitihani yao ya kidato cha nne skuli ya Sekondari Mkanyageni Wilaya ya Mkoani, Mratib wa kitengo cha elimu ya watu wazima Pemba Salim Kuza Sheikhan amesema, ni muhimu kwa wanafunzi hao kujipangia mustakbali wa maisha yao ya mbeleni na kuzingatia ushauri wanaopatiwa na wazazi wao.

Wanafunzi wa skuli ya Secondary Mkanyageni Wilaya ya Mkoani

Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa na mashirikiano na walimu katika kuleta maendeleo bora na imara katika sekta ya elimu sambamba na kuwa karibu na watoto wao kuhakikisha hawakiuki sheria za nchi.

Akigusia suala la kujiendeleza kwa wanafunzi ambao hawatobahatika kuendelea kidato ch tano na sita  amesema ni vyema kwa wazazi kuwapeleka vituo vya mafunzo ya amali ili katika fani mbali mbali zinazosomeshwa vituoni humo.

Kwa upande wake mwalim Mkuu wa Skuli ya Mkanyageni Sekondar Mbarouk Suleiman Abdallah amewataka wazazi na walezi  kuendeleza mashirikiano baina yao,wanafunzi na walimu ili kuleta mabadiliko makubwa ndani ya sekta ya elimu nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya wanaharakati wa kupinga vitemdo vya udhalilishaji wa kijinsia wilaya ya Mkoani, Machano Ame Faki amewataka wanafunzi hao kutojihusisha na vitendo viovu vikiwemo vya udhalilishaji wa kijinsia na badala yake kuwa wakala wazuri katika jamii inayo wazunguka.

Akitoa nasaha kwa niamba ya wazazi wenzao Hafidha Mohammed Khalfan na Ustadhi Haji Ali Shaali wamewataka wanafunzi hao kutokukata tama ya kujiendeleza kimasoma kwa wale ambao hatopata matokeo mazuri sambamba na kuyafanyia kazi yale mazuri ambayo wameyapata skulini hapo na wasimpe njia bilisi katika kufanya maovu kwa shetani humpoteza mtu katika njia mbaya.

Jumla ya wanafunzi 86 wamehitimu masomo ya ya elimu ya lazima wakiwemo wanakwake 50 na 36 ambapo wanafuzi wa masomo ya sayansi  41 na masomo ya sanaa  46, yakiwa ni Mahafali ya nne kufanyika skulini hapo