Mkoani FM

Early Madrasa Childhood: Kuwapa elimu ya utetezi watu wenye ulemavu

26 November 2022, 8:38 am

 

Wardat Mahmoud Mussa kutoka Jumuiya ya watu wenye ulemavu Pemba

Watu Wenye Ulemavu Kisiwani Pemba wamesema elimu waliyopatiwa kutoka taasisi ya Early  Madrasa Childhood imeweza kuwasaidia kuwajengea uwelewa wa kiutetezi katika kupata haki zao kisheria.

Akizungumza Maryam Juma Kombo kutoka Taasisi ya Usalama Barabarani  amesema  kupitia elimu hiyo ameweza kujiamini zaidi ukilinganisha na hapo awali jambo linalosaidia katika harakati zake za kila siku.

Saida Amour mratibu wa mradi wa Maendeleo Jumuishi ya Jamii Community Based Inclusive Development (CBID) kutoka Early Madrasa  ChildHood  amesema lengo la mradi huu ni kuongeza uwelewa kwa watu wenye ulemavu juu ya simamia haki zao za msingi katika nyanja mbalimbali.

Salma Haji Sadati mkufunzi Mkuu wa mradi katika kuwajengea  watu wenye ulemavu amesema   Misingi ya maendeleo ni uchambuzi wa Sera na Sheria hivyo ni vyema kwa waliopata fursa ya kufikiwa na elimu hii  waitumie vizuri lengo ni kuona kwa namna gani yale yaliyosahauliwa yanawafikia na kupata  ushawishi wa kiutetezi.

Simon Meigaro Moikan Mkurugenzi Mkaazi kutoka shirika la Agakhan

Simon Meigaro Moikan Mkurugenzi Mkaazi  kutoka shirika la Agakhan Tanzania amesema shirika limeweza kuiwezesha taasisi ya Early ChilHood kuwafikia kundi hilo lengo ni kuongeza nguvu katika kulifikia kundi hilo kwa njia jumuishi ili watu wenye ulemavu  kupatiwa fursa sawa kwenye harakati za maendeleo.

Malengo17 ya Dunia ya maendeleo endelevu  ameeleza kuwa ushawishi na utetezi wa haki za watu   wenye Ulemavu   na kupata fursa  sawa kama watu wengine hapa visiwani Zanzibar