Mkoani FM

IUCN kupitia ubalozi wa Ireland Tanzania yang’arisha vikundi vya wajasiliamali Pemba

20 August 2022, 10:44 am

Warda Faki Fafari akiwasilisha Ripoti ya kikundi chao.

Wanavikundi cha Uvumbuzi Pujini Kibaridi,Mapape Cooperative Chambani na Yataka Moyo Chokocho wamelishukuru Shirika la IUCN kupitia mradi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland Tanzania kwa kuwasadia kwa hali na mali katika kuboresha vikundi vyao.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa ripoti fupi mara baada ya kufikiwa na ugeni wa Mkuu wa Mkoa uliombatana na wadau kutoka IUCN Fatma Haji Zarali kutoka ushirika wa Uvumbuzi wanaojishuhulisha na uzalishaji wa Chumvi, ukulima wa mboga mboga na uhifadhi wa mikoko amesema mradi huo umeweza kuwakomboa kwa kiasi kikubwa kwani kwa sasa miundombinu yao ipo imara,elimu ya uzalishaji bora na salama kwa mtumiaji,soko la uhakika hali iliyochangia kuongeza uzalishaji kutoka tani 4 hadi kufikia tani 20 kwa mwaka.

Kwa upande wa Mapape Cooperative wamesema kikundi chao kinajishuhulisha na ufugaji wa majongoo bahari, kaa,nyuki na uhifadhi wa mikoko ambapo kwa sasa wana jumla ya majongoo bahari 2700,zaidi ya kaa 250,na banda la kufugia nyuki lenye uwezo wa kuchukua mizinga 60 sambamba na kupeleka  chuo cha bandari majongoo 20 kwa lengo la kufanyia utafiti na wakutotolesha vifaranga ili kufaidika na ufugaji huo.

Ameongeza pia kupitia mradi huo kumepatikana ajira 40 kwa jamii iliyowazunguka iliyojumuisha vijana wazee wa kike na kiume hali inayounga mkoano juhudi za serikali katika kukuza uchumi wa buluu na ajira kwa vijana na wazee.

Nao wanakikundi cha Yataka Moyo Chokocho wameushukuru Ubalozi wa Ireland Tanzania kupitia shirika la IUCN kwa ufadhili wa kuanzisha shamba mseto wa kilimo cha mwani na ufugaji wa majongoo na kupata mafunzo yaliosaidia kuongeza uzalishaji ukilinganisha na mavuno ya awali .

Dr, Elinas Monga Mwakilishi kutoka IUCN

Akitaja lengo la Program ya ustahamilivu wa pwanani na bahari  pia ni Mwakilishi kutoka IUCN  Dr, Elinas Monga amesema ni kusaidia kukuza uchumi wa buluu kupitia uhifadhi shirikishi wa mifumo mikuu ya ikolojia na baionuai hali itakayosaidia utekelezaji mzuri wa sera ya uchumi wa buluu.

Dr, Monga  ameeleza Program yao kwa sasa inafanya kazi na  vikundi  vinne viwili Pemba na viwili kutoka Tanga  na kuwapa mafunzo ya ujasiriamali  na kila kikundi kimepatiwa  Tsh 29,000,000. Ikiwa ni ruzukuwa  kwa utekelezaji wa mpango biashara ambao utaboresha na kukuza biashara zao

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja amewaeleza wanuafaika wa mradio huo kutumia vizuri fursa walizozipata na kuwa wabunifu wa shunguli nyengine zilizopo kwenye sekta ya uchumu wa bluu sambaba na kuendelea na shughuli zao hata baada ya kumalizika  kwa mradio.

IUCN  ni shirika la kimataifa linalojiusisha na uhifadhi wa maeneo asili ni shirika la wanachama na kwa sasa lina jumla ya washirika wanachama 1400 Duniani kote na linatekeleza program mablimbali ikiwemo Mabadiliko ya Tabianchi,Uhifadhi wa rasilimali maji,Masuala ya jinsia katika uhifadhi wa mifumo ya ardhi na ustahamilivu wa pwani na bahari, kwa sasa Pemba  inatekeleza program ya ustahamilivu wa uhifadhi wa bahari iliyoanza mwezi wa tisa mwaka 2021 kwa ufadhili wa Ubalozi wa Ireland Tanzania.