Mkoani FM

Watahaniwa kidato cha 4 Mkanyageni Pemba watakiwa wasiwe wadanganyifu.

23 October 2021, 2:02 pm

Wanafunzi wa skuli ya Mkanyageni Pemba

Na Khadija Ali Yussuf

Watahiniwa kidato cha nne Skuli ya Mkanyageni Sekondari wametakiwa kuwa makini na kuacha udanganyifu wakati wa ufanyaji wa mitihani yao ya taifa.

Ushauri huo umetolewa na Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Mbarouk Suleiman Abdallah wakati wa Mahafali ya kuwaaga wanafunzi hao yaliyofanyika katika skuli ya Mkanyageni amesema ni vyema kuwa na nidhamu ndani ya chumba cha mtihani ili kuepusha usumbufu .

Wakisoma risala wanafunzi hao wamesema wanakabilikwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya maabara, ukosefu wa waalimu wa sayansi pamoja na kutokuwepo kambi za wanafunzi hali inayosababisha kuzorotesha ukuwaji wa elimu na matayarisho Mazuri ya kuikabili mitihani yao ya taifaWakati huo huo Wamewashauri wanafunzi wenzao ambao bado anaendelea na masomo maskulini hapo kuwa makini katika kutumia fursa ya elimu kwa kufuatilia masomo pamoja na kuwasikiliza waalimu wao ili kupata mafanikio imara ba ardhi za walimu wao.

Akikamribisha mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli hio Idrisa Omar amewapongeza waalimu wa msingi kwa kuwajengea uwezo wanafunzi na kuwataka wasisite kutafuta elimu baada ya mtihani yao kwani ndio msingi wa maisha.Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Mohd Faki Saleh amesema kutokana na changamoto zilizotajwa kupitia risala ya wanafunzi ameahidi kuwa balozi wa kuziwasilisha sehemu husika sambamba na kuwataka kuwa na mawazo ya kusoma masomo ya sayansi ili kusaidia serikali na taifa kwa ujumla.

Mgeni rasmi Moh’d Faki Saleh akitoa nasaha kwa wanafunzi wa skuli ya Mkanyageni

Akigusia uwepo wa janga la corona amesema ni vyema kwa wanafunzi na jamii kuendeleza kuchukua tahadhari ya kujikinga na maradhi hayo ili kulinda afya zao.Kwa upende wake Afisa Elimu Wilaya ya Mkoani Salum Kuza Sheikhan Amewaahidi wanafunzi hao zawadi kwa atakaepata Daraja la kwaza na la pili kwa lengo la kuongeza nguvu ya usomaji hali itakayopelekea ufaulu mzuri na kuijengea sifa mzuri skuli yao na kuwa mfano wa kuigwa.

Jumla ya watahaniwa 141 wa Skuli ya Sekondafi Makayageni wanategemea kufanya mitihani ya taifa yaani NEC mwezi ujao ambapo 96 ni sayansi na 45 ni elimu ya sanaa (Art).