Mkoani FM

Wizara ya afya watakiwa kutoa elimu ya chanjo vijijini

9 October 2021, 8:14 am

Kutokuwepo kwa elimu ya kutosha kwa baadhi ya vijiji ni changamoto inayopelekea kushindwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa korona.

Mwandishi wa Mkoani FM akizungumza na mmoja ya wanajamii kutoka wilaya ya Mkaoni kuhusu uwelewa wa chanjo ya corona

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti wananchi  wa wilaya ya mkoani wamesema ni  vyema  wizara  ya  afya iweke utaratibu  wa  kuwafikia  wananchi  hususani  wa  vijijini  ili  kuwapatia  elimu  hiyo .

Sauti za wanajamii wa wilaya ya Mkoani wakieleza kutokua na elimu ya chanjo ya corona

Kwa upande wao baadhi ya masheha  wamesema ipo haja kwa jamii kupatiwa elimu ya kujilinda na corona ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza.

Afisa Mdhamin wizara ya Afya Pemba Yakuob  Mohammed Shoka amesema wamejipanga kutoa elimu kwa kushirikiana na kitengo cha elimu ya afya kwani bado wanakazi kubwa ya kuelimisha jamaii juu ya wimbi la tatu la korona na kuitaka jamii kuwa tayari kufuata yale maelekezo yote wanayopewa na wataalamu  wa afya.

Sauti ya afisa mdhamini wizara ya Afya Pemba

Sambamba  na  hayo  wameiomba  wizara  husika kupatiwa elimu ya ugonjwa huo ili waweze kushirika kikamilifu  ktika  zoezi hilo  bila ya kuwa na hofu.