

28 September 2021, 10:28 am
Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba ACP Richard Tadei akitoa maelezo juu ya watuhumuwa wa madawa ya kulevya
Na Amina Ahmed
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limefanikiwa kukamata jumla ya kete 350 za madawa ya kulevya aina ya heroini yaliyokuwa yakiuzwa kwa vijana wanaotumia na kuwashikilia watu wawili wakihusika na biashara hiyo haramu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba ACP Richard Tadei Mchovu amewataja waliokamatwa na madawa hayo kuwa ni Ali Mjawiri mwenye umri wa miaka 40 mkaazi wa Madungu ambaye alikamatwa maeneo ya Africana na mwengine ni Said Moh`d (30) mkaazi wa Minazini Chake Chake.
Aidha Kamanda Mchovu amesema katika operesheni ya usalama barabarani wiki hii jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba imekamata jumla ya pikipiki 65 kwa makosa mbali mbali ikifemo kutokuwa na leseni, bima, na makosa ya kutovaa helment kwa madereva au abiria.