Micheweni FM

PEGAO, TAMWA ZNZ, ZAFELA zaahidi kuendelea kutetea ushiriki wa wanawake katika uongozi.

1 October 2021, 7:47 am

Mkurugenzi wa PEGAO Hafidhi Abdi Said akizungumza na wananchi hawapo pichani katika kijiji cha Kinyikani.

Na Gaspary Charles.

Jumuia ya  utetezi  wa kijinsia na mazingira  pemba(  Pegao)  imesema  itaendelea kushirikiana   na wanawake  wote wanaotaka kugombea nafasi za uongozi katika kutatua changamoto zinazowarudisha nyuma kufikia lengo hilo  katika nyanja mbali mbali za siasa, democrasia na uchumi

Ameyasema hayo Mkurugenzi wa  Jumuia hiyo Pemba Hafidh Abdi Said katika mkutano maalum wa uhamasishaji jamii  juu ya wanawake kudai haki za uongozi uliofanyika kinyikani mchangamdogo mkoa wa kaskazini pemba.

Amesema endapo wanawake watakuwa na dhamira  ya kugombea nafasi za uongozi na kukutana  na changamoto jumyia hiyo itasaidia kulitimiza  lengo hilo  ili fursa hiyo kwa muda stahiki.

 Wakizungumza katika mkutano huo wahamasishaji  jamii kutoka pegao Akiwemo Rukia Ibrahim, amewataka wanawake hao waliohudhuria katika mkutano huo  kuwa mabalozi kwa wanawake wengine katika jamii juu ya kudai haki zao za uongozi katika nyanja zote.

Nao baadhi ya wanawake  wa shehia ya  kinyikani  wameiomba pegao kuendela kuwahamisha  kupata uzoefu wa kuondoa woga wa kudai haki zao za kuwa viongozi ili wajikomboe katika maendeleo pamoja na kuwapatia elimu kuhusu uongozi  pamoja na kuwajengea uwezo  juu ya suala hilo.

Aidha wameeleza kuwa   changamoto  kubwa zinazowakabili wanawake hao ni kukosa  kujiamini wanapodhamiria kugombea kutokana na  kukosa uzoefu wa kuzngumza  na kudai haki zao mbele ya   makundi ya watu  majukumu mengi ya familia wanayoachiwa na wanaume.

 Jumuia ya pegao inatekeleza  mradi wa  uhamasishaji jamii juu ya wanawake kudai nafasi za uongozi kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa  Zanzibar  pamoja na Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Zafela.