Mazingira FM

Wenyeviti wa mitaa 88 Halmashauri ya Mji wa Bunda watishia kujiuzulu

13 May 2023, 5:24 pm

Ofisi za ccm wilaya ya Bunda

Wenyeviti wa mitaa 88 Halmashauri ya Mji wa Bunda watishia kujiuzuru waandamana kuelekea ofisi za Chama CCM wilaya.

Tukio hilo la aina yake limetokea 12 May 2023 wilayani Bunda ambapo wenyeviti hao walionelana kuitaji uongozi wa chama huku wakiwa wamebeba mihuri yao kwa lengo la kuikabidhi kwenye chama na kuachana na nyadhifa hizo

Wakizungumza na Mazingira Fm wenyeviti hao wamesema kwa muda sasa hawatendewi haki na Wala hawathaminiwi, hawapewi stahiki zao.

“Sisi ni wenyeviti lakini haki zetu hatupewi viongozi wa serikali ngazi ya Halmashauri na Wilaya hawatambui uwepo wetu maana hawajawahi kukutana na sisi tunajitolea mambo mengi ya kijamii tulihamasisha Sensa mambo yakaenda vizuri, tulihamasisha anwani za makazi mambo yakaenda vizuri, kampeni za chanjo za serikali tunahamasisha lakini viongozi wa Halmashauri wamekuwa hawataki kutupa stahiki zetu sasa tumechoka”

Wenyeviti hao wamesema mwanzoni walikuwa wakilipwa shiling elfu 50,000 kwa mwezi kipindi Cha Mkurugenzi Janeth Mayanja lakini alipoondoka hela hiyo ikazuiliwa kwa sasa wanapata elfu 5,000 kwa mwezi

” Mwanzoni kipindi Cha Mkurugenzi Janeth Mayanja ambaye kwa sasa ni DC Hanang na Mkuu wa Wilaya Lydia Bupilipili tulikuwa tukilipiwa Hadi ofisi tunapofanyia kazi pia tulikuwa tunakutana nao tunashirikishwa kila kitu kwenye mitaa yetu lakini tangu waondoke hayo yote yameisha saizi eti Mkurugenzi anatulipa elfu 5,000 kila mwezi sasa hii ya nini itatosha nini wakati Mayanja alikuwa anatulipa elfu 50,000 tumeandika barua kwenda kwenye chama mwezi wa 2 kutaka kujiuzulu sasa tumekuja kuonana na viongozi wa CCM wilaya ili tukabidhi mihuri”

Kupitia Katibu wa Siasa na uenezi CCM wilaya ya Bunda Ndugu Gasper Charles aliyepokea maandamano hayo aliwataka wenyeviti hao kuwa watulivu kwa kuwa malalamiko yao yameshafika ofisini

Aidha aliwaomba kufika siku ya jumatatu 15 May 2023 Ili chama kiweze kuwasikiliza madai yao

“Naomba muwe watulivu punguzeni jazba bahati Nzuri nyote mitaa 88 mnatokana na chama Cha mapinduzi sasa sisi kama chama hatuko tayari kuona mnajiuzulu pia hatuko tayari kuona mnakosa stahiki zenu mmefanya vizuri kukimbilia kwenye Chama niwaombe kwa kuwa katibu wa Chama Wilaya amewataka mfike jumatatu nami naungana naye kuweni na subra Jumatatu Asubuhi saa tatu njooni Chama kitawasikiliza” alisema Gasper