Mazingira FM

DC Naano akiri Bunda kuwa kinara wizi miradi ya maendeleo mkoani Mara

26 April 2023, 9:58 am

Wilaya ya Bunda imeadhimisha miaka 59 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya kongamano kubwa huku mgeni rasmi akiwa ni Mhe Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano.

Kongamano hilo limewakutanisha viongozi wa taasisi za serikali na wakuu wa taasisi binafsi, Waheshimiwa Madiwani wazee maarufu miongoni mwa wageni wengine.

Akizungumza katika kongamano hilo mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Dkt Naano amesema Kuna mambo mengi ya kujivunia kutokana na uwepo wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni pamoja na uhuru wa kwenda katika sehemu hizo mbili bila kikwazo na kufanya kazi, kusaidia kukuza uchumi, pamoja na fulsa za kibiashara.

Aidha Dkt Naano amewataka vijana na wakazi wa Bunda kuwa wazalendo katika kuhakikisha Bunda inapata Maendeleo huku akikemea suala la Wizi wa Fedha za miradi ya Maendeleo ambapo amekiri wazi kauli ya Mhe Mkuu wa Mkoa aliyoitoa hivi karibuni kuwa Bunda inaongoza kwa Wizi wa Fedha za miradi ya Maendeleo kwa mkoa wa Mara.

DC Vicent Naano

Awali akizungumza katika Kongamano hilo Katibu wa Siasa na uenezi CCM wilaya ya Bunda ndugu Gasper Charles amesema wao kama chama wanaipongeza serikali katika kutekeleza ilani waliyowapatia yenye kurasa 303 ya mwaka 2020 Hadi 2025

Gasper Charles

Kwa upande wao wananchi wameipongeza Serikali kwa kuuenzi muungano huu ambayo ndiyo tunu ya waasisi wa Taifa hili walioiacha