Mazingira FM

BUNDA QUEENS YAREJEA KWA KISHINDO NA KUPOKELEWA NA MKUU WA WILAYA DKT. VICENT ANEY

26 April 2023, 9:21 am

Mabingwa wa ligi Daraja la kwanza wanawake Bunda Queens yarejea nyumbani kwa kishindo na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya pamoja na mamia ya wakazi wa Bunda katika uwanja wa sabasaba.

Bunda Queens kwa heshima ya waliyoileta Bunda wamemkabidhi Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Kikombe cha ushindi ambacho wamekinyakua katika mashindano ya ligi Daraja la kwanza yaliyofanyika jiji Mwanza na kufuzu kupanda ligi Kuu ya wanawake Serengeti Lite kwa msimu ujao.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameipongeza timu hiyo na kuahidi kuwapatia shilingi milioni moja na laki tatu ambazo atazikabidhi katika hafla ya kuwapongeza itakayofanyika hivi karibuni.

Aidha, Mhehimiwa Mkuu wa Wilaya ameahidi kukiwasilisha kikombe hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo amesema ataambatana na timu hiyo siku ya kwenda kukabidhi.

Ikumbukwe kwamba Bunda Queens ndio timu pekee ya Mkoa wa Mara kupanda ligi Kuu ya wanawake Tanzania bara Serengeti Lite hivyo wanapeperusha bendera ya Mkoa mzima.

Manthalani, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameahidi kuukarabati uwanja wa sabasaba kwa kushirikiana na wamiliki na wadau mbalimbali ili kuuweka katika ubora unaotakiwa ili tuweze kushuhudia mtanange wa ligi kuu mubashara katika dimba hili.

chanzo Bunda Tc

kaziiendelee