Mazingira FM

Bunda; Suala la maadili latiliwa mkazo kwenye Swala ya Eid El Fitr.

22 April 2023, 6:56 pm

Waislam wilayani Bunda wameungana na wezao kote Duniani kusherekea Sikukuu ya Eid El Fitr ikiwa ni kukamilisha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan miongoni mwa Nguzo kuu tano za uislam

Katika ujumbe wake Sheikh Mkuu wa Bunda shekhe Abubakar Zuber Bin Nyambuga amewaasa waumini wote wa kiislam kutoa zaka na sadaka kwa watu wenye uitaji na kuondoa choyo miongoni mwa wenye Mali.

Pamoja na wito huo Sheikh Abubakar amewaasa wazazi na walezi kuzingatia maadili kwa watoto wao kutokana na kuzuka kwa vitendo vya Ukatili kwenye Jamii ikiwa ni pamoja na matukio ya ushoga na ndoa za Jinsia Moja ambayo kiimani ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu.

Shekhe Abubakar Zuber

Kwa upande wake Fatuma Khamis maarufu mama Ushungi amesema wanamshukuru Mwenyezi Mungu kumaliza Mfungo huu wa Ramadhan na leo wanasherekea Eid El Fitr wakiwa na Afya njema.

Akizungumzia ujumbe uliotokewa na kiongozi wa ibada amesema suala la Maadili ni jukumu la wazazi, walezi na Jamii nzima kwa Ujumla.

Amesema sababu ya kuporomoka kwa maadili ni wazazi kukosa muda wa kukaa na watoto wao kwa kuwa saizi wazazi wengi wajielekeza kwenye utafutaji huku wakisahau malezi kwa watoto.

Fatuma Khamis