Mazingira FM

Wazazi waaswa kuwalea watoto katika maadili mazuri ili kuepukanana na masuala ya ushoga

14 April 2023, 12:07 pm

Leo ikiwa ni tarehe 13 mwezi wa 4 kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wazazi Wametakiwa Kuwalea Watoto Katika Maadili Mazuri  ili Kuepukana Na jamii isiyofaa.

Hayo yamesemwa katika ufunguzi wa wiki ya kuzienzi falsafa za baba wa taifa ulioandaliwa na taasisis ya Mwl Nyerere Faundation iliyofanyika wilayani Butiama mkoani Mara na kuudhuriwa naviongozi mbalimbali.

akizungumza katika kongamano hilo la ufunguzi mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe DrĀ  Vicent Anney Naano amesema kazi kubwa ya baba wa taifa aliyoifanya kwa taifa la Tanzania haiwezi kusahaurika akizungumzia suala la kuondoa ukabila miongoni mwa watanzania.

Dr Vicent Naano

Naye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya taasisi ya Mwalimu Nyerere Faundation Joseph Warioba Butiku amesema mkoa wa Mara ndiyo uliomzaa Baba wa Taifa ambapo misingi ya kiongozi huyo ilikuwa ni utu, usawa na haki na ndivyo vilivyoleta amani na kama watu wa Mara hawaviamini wanaamini nini?.

Joseph Matiko Butiku

Naye mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Butiama ambaye pia ni naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Jumanne Sagini amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani imeendelea kuzienzi falsafa za baba wa taifa kwa kutekeleza miradi ambayo ilikuwa ndoto ya baba wa taifa kama vile bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere, serikali kuamia Dodoma, ujenzi wa hospitali ya kwangwa musoma na ukamilishwaji wa barabara ya makutano sanzate kwa kiwango cha lami.

Aidha ameongeza kuwa ni jukumu la wazazi na walezi kwenye jamii kuwalea watoto katika maadili Mazuri kwa ajili ya kizazi kijacho na kuwaepusha na mambo mabaya ikiwemo ndoa za jinsia moja na masuala ya ushoga huku akisema serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaodhibitika kujihusisha na masuala ya ushoga.

Mhe Jumanne Sagini