Mazingira FM

Magwayega;. Jumuiya ya wazazi ccm tutaendelea kusimamia nguzo zetu ambazo ni Afya, Elimu, Mazingira na Maadili

28 March 2023, 10:37 am

Mwenyekiti wa wazazi CCM wilaya ya Bunda ndugu wakili Leonard Magwayega amesema suala la Maadili Elimu Mazingira na Afya wataendelea kuvisimamia kwa kuwa ndiyo nguzo za jumuiya ya wazazi.

Ndugu Magwayega ameyasema hayo katika ziara ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM taifa Ndugu Fadhili Rajabua Maganya aliyoifanya wilayani Bunda.

LEONARD MAGWAYEGA

Katika ziara hiyo Ndugu Maganya ametembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo kupitia kwa diwani wa kata hiyo Flaviani Chacha Nyamageko ameshukuru jitihada za serikali kusogeza huduma ya afya  karibu na wananchi wake kwa kuwa walikuwa wakiteseka.

FLAVIAN CHACHA

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Anney Naano amesema serikali wilayani Bunda inaendelea kusimamia ilani ya CCM kwa kuendelea kusimamia miradi inayoletwa wilayani hapo.

DR,. VICENT NAANO

Naye mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi taifa amesema ni jukumu la chama ni kuisimamia serikali kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa kwa kuwa ilani inayotekelezwa na serikali ni ya CCM huku akiwatupia lawama wabunge wa wilaya ya Bunda kwa kushindwa kushiriki kwenye shughuli za chama.

FADHIL RAJABU MAGANYA