Mazingira FM

Wakazi wa Nyatwali nimewasikia tegemeeni mazuri kutoka serikali ya CCM ; Rajabu Maganya Mwenyekiti Wazazi CCM taifa.

25 March 2023, 7:51 pm

Mwenyekiti wa wazazi CCM taifa Ndugu, Fadhil Rajabu Maganya ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu CCM taifa amesema kero za wakazi wa kata ya nyatwali amezisikia na wategemee majibu mazuri kutoka serikali inayotokana na chama cha mapinduzi.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake wilayani Bunda leo 25 march 2023 ikiwa ni siku ya tano ndani ya mkoa wa Mara.

Ndugu Maganya amesema jambo la Nyatwali kama ambavyo limesemwa na viongozi mbalimbali kunzia ngazi ya  wilaya mkoa na hatimaye limefika kwake  na  kwa nafasi yake kama chama kinachosimamia serikali na utekelezaji wa ilani amelichukua.

RAJABU MAGANYA

Katiaka kuwasilisha kero za wakazi wa Nyatwali kwa niaba ya wananchi diwani wa kata ya Nyatwali Mhe Malongo Mashimo amesema tatizo kubwa ni fidia ndogo, malalamiko ya eneo la mjapani, eneo la malisho, maeneo yaliyozama kwenye maji miongoni mwa kero zingine.

MALONGO MASHIMO

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafugaji taifa Mhe Mlida Mshota amesema suala la tathmini ndani ya kata ya Nyatwali haliendi sawa hasa katika uwiyano wa ghalama za wananchi walizozitumia na ghalama halisi baada ya tathimini hivyo amemuomba mwenyekiti wa wazazi kulibeba jambo hilo la Nyatwali.

MLIDA MSHOTA

Naye katibu wa jumiya ya wazazi mkoa wa Mara Ndugu Langaeli Akyoo amemshukuru mwenyekiti wa wazazi taifa kwa kuwasikiliza wakazi wa Nyatwali lakini ameitaka serikali kuliangalia vizuri suala la Nyatwali ili baadae kusije kutengenezwa masikini au ombaomba wa baadae hivyo jambo hilo lisipelekwe harakaharaka.

LANGAELI AKYOO

Katika ziara hiyo mjumbe huyo wa kamati kuu CCM taifa pia ametembelea miradi mingine ikiwa ni mradi wa ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Kabasa ambapo ameweka jiwe la msingi, mradi wa ujenzi wa madarasa shule ya sekondari sazira na mradi wa ujenzi wa Hospitali Ya Halmashauri Ya Mji Wa Bunda katika kata ya Bunda Stoo.