Mazingira FM

CHADEMA; Wampa tano Rais Samia kuruhusu mikutano ya hadhara.

19 March 2023, 7:23 pm

Salumu Mwalimu

Naibu Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Zanzibar SALUMU MWALIMU amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Kiongozi huyo wa CHADEMA ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Bunda mjini.

Akiwa ameanbatana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo aliyekuwa mbunge wa iringa mjini Peter Msingwa, aliyekuwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje, pamoja na viongozi wengine wa kimkoa na kikanda kutoka cha cha demokrasia na maendeleo chadema.

Mwalimu amesema ni jambo la busara lililofanywa na Rais huyo wan chi kwa kuruhusu mikutano ya hadhara ambapo wananchi wanapata fulsa ya kusikiliza serana hoja za kila chama kisha wananchi wenyewe kuamu ni lipi bora kwao.

Aidha kupitia kwa Peter Msigwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Iringa mjini amesema kuhusu kauli ya Lema kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda haikuwa na lengo la kubagua bali ilikuwa na lengo la kuonesha kundi hilo la vijana limelazimika kuingia kwenye kazi hiyo kutokana na kukosa kazi maalumu ya kufanya.

peter Msigwa