Mazingira FM

Polisi Bunda watembelea wagonjwa hospitali ya Bunda DDH kuonesha matendo ya huruma.

11 March 2023, 2:08 pm

Jeshi la polisi wilaya ya Bunda mkoani Mara wametembelea na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa hospitali ya Bunda DDH ikiwa ni siku ya familia kwa jeshi hilo yenye kauli mbiu ( Bunda Family Day Tushirikiane Kutokomeza Uharifu )

Mrakibu wa polisi Mashaka Ikwabe OCD Bunda

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa wagojwa Mkuu wa Polisi Bunda  Mrakibu wa polisi Mashaka Ikwabe amesema wameamua kwenda kuwaona wagonjwa Hospitalini hapo ikiwa lengo ni kuonesha matendo ya huruma lakini pia kuionesha jamii ushirikiano katika kupambana na uharifu .

Aidha ameongeza kuwa polisi ya  sasa ni tofauti na zamani hivyo wananchi wanatakiwa kuelewa na kushirikiana nao katika kutokomeza masuala ya ukatili na unyanyasaji kwenye jamii.

mrakibu wa polisi MASHAKA IKWABE OCD BUNDA

Naye daktari kiongozi wa hospitali hiyo Dr Pendo Faustine amesema wamepokea msaada huo kwa mikono miwili  kutoka jeshi la polisi wilayani Bunda na wamekuwa na mchango mkubwa katika kuonesha ushirikiano baina yao na hospitali  pia wameongeza imani kwa wateja wao hasa katika kuonesha matendo ya huruma kwa kuleta zawadi kwao, kuimalisha ulinzi na usalama hasa kwa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili unaofanyika katika jamii.

Dr Pendo Fastine
DR PENDO FAUSTINE, DAKTARI KIONGOZI BUNDA DDH

Naye lucas Daniel mkazi wa Bunda ambaye pia ni mdau wa jeshi la polisi ameitaka jamii kuacha kuogopa kushirikiana na jeshi hilo  ili kusaidia kutambua waarifu katika maeneo yao.

Lucas Daniel Mkazi wa Bunda
LUCAS DANIEL MKAZI WA BUNDA