Mazingira FM

DC Naano: Maslahi binafsi, usimamizi duni, ni miongoni mwa sababu za mapato ya halmashauri Bunda DC kushuka.

10 March 2023, 12:52 pm

DKT. VICENT NAANO, DC BUNDA

Mkuu Wa Wilaya Ya Bunda Daktari Vicent Naano Anney Amesema Kuwa Changamoto Nyingi Zilizopo Katika Halmashauri ya wilaya ya bunda Zinatokana Na Usimamizi Duni wa Watendaji Unaosababishwa Na Watu Kupenda Maslahi Yao Binafsi Suala Linaloaibisha Taasisi Ya Saerikali.

Hayo Ameyasema Katika Kikao Cha baraza La Madiwani Cha Kujadili Taarifa Ya Robo Ya Pili mwaka Wa Fedha 2023–2024 Wa Halmashauri Kuwa Watendaji Wengi Wa Halmashauri Wamekata Tamaa Hali Inayochangia Utendaji Kuwa Mbovu Ambapo Amewaasa Watendaji Hao Waachane Na Dhana Potofu Kwamba Wakihama Halmashauri Hiyo watafanya Vizuri Badala Yake Wabadilike Wawe Na Hali Ya Utendaji Kazi.

DC. DR VICENT NAANO

Aidha Amesema Kuwa Jumla Ya Watoto 569 Hawajaripoti Shuleni Ambapo Amemwagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri Hiyo Kwa Kushirikiana Na Watendaji Wengine Kushughulikia Suala Hilo Ikiwezekana Wazazi Wa Watoto Hao Wakamatwe.

Amesema Matokeo Mabaya Kwa Shule Za Sekondari Yanachangiwa Na Changamoto Ya Upungufu Wa Madawati, Utoro, Usimamizi Mbovu, Mbinu Mbovu Za Ufundishaji Na Utungaji Wa Mitihani Ya Ndani.

Mkuu Huyo Wa Wilaya Amewataka Pia Watendaji Waache Tabia Ya Kukaa Maofisini Bila Shughuli badala yake waende Wakakusanye Ushuru Na Tozo Mbalimbali Ambazo Zitachangia Kuogeza Mapato Ya Halimashauri Pia Waongeze Beria Katika Maeneo Ya Nyabikere Kata Ya Nyamuswa, Kisorya, Ketare Na Kyandege Ambapo Lengo Ni kufikia Asilimia Themanini Ya Mapato Kwa Mwaka Wa Fedha 2023—2024.