Mazingira FM

Wanawake BUWASSA Bunda waadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada

8 March 2023, 11:54 am

Wafanyakazi wanawake wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira bunda BUWASA wamesherekea siku ya wanawake duniani kwa kutoa vitu mbalimbali kwa watoto wahitaji na kutembea wodi ya  mama waliojifungua hospitali ya Bunda DDH

Akizungumza  katika siku hiyo kaimu mkurugenzi wa BUWASA  Ester Giryoma amesema wao kama wanawake ndani ya mamlaka inayotoa huduma kwa jamii wameona ni vema kutoa sadaka hiyo ili kuionesha jamii kwamba waka pamoja nao

ESTER GIRYOMA KAIMU MKURUGENZI BUWASSA

Katika maadhimisho hayo pia waliwaalika viongozi wa dini ambapo kupitia kwa mchungaji Elikana Magigita ambaye ni mwenyekiti  wa CCT Bunda  ameasema jambo lililofanywa na wanawake kutoka mamlaka ya maji Bunda ji jambo la kibiblia hivyo anaamini Mungu atazidi kuwapa Baraka kwa kadri walivyojitoa

MCHUNGAJI ELIKANA MAGIGITA, MWENYEKITI CCT BUNDA

Naye mwakirishi wa shekhe wa wilaya ya Bunda ostadhi Adiru Ayubu  amewataka wanawake wa  mamlaka ya maji bunda kutokuacha kuwasaidia wahitaji kwa kuwa kadri wanavyotoa ndivyo wanavyozidi kubarikiwa

OSTADHI ADIRI AYUBU

Naye katibu wa hospitali ya Bunda DDH Dr Pendo amesema anawashukuru wanawake wa mamlaka ya maji kuja kutembelea hospitali hiyo na kuwaona akinamama wenzao waliojifungu a lakini na watoto wanaopata matibabu kartika hospitali hiyo maana wangeamua kwenda sehemu nyingine lakini wameona inafaa kwenda hapo na kuahidi kugawa msaada huo ulioletwa kama ilivyokusudiwa

DR. PENDO KATIBU WA HOSPITALI YA BUNDA DDH